Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe lawataka Watendaji wa Kata kusimamia ukusanyaji wa Mapato kikamilifu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mhe.Valentino Hongoli leo Novemba 01, 2023 kwenye Baraza la kujadili taarifa za kata.
Katika Baraza hilo amewata Watendaji hao kutekeleza makubaliano ya kuhesabu Mbao kwa kuzingatia kila ubao kuwa hiyo itakuwa ni moja ya mbinu nzuri ya kulinda Mapato ya Halmashauri.
"Mapato yote yanayopatikana katika Kata na vijiji ni Mali ya Halmashauri hivyo basi umakini mkubwa unahitajika Ili kuhakikisha hakuna chochote kinachopotea".Alisema Mhe.Hongoli
Aidha,Ameongeza Kwa kusisitiza ushirikiano katika utendaji kazi ikiwa ni Moja ya kuunga mkono jitihada za Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Nae, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ndugu.George Makacha ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuyafanyia kazi yale yote yalioagizwa hususani suala zima la kukusanya na kulinda Mapato.
Baraza hilo la kawaida limekuwa na dhumuni kubwa la kujadili masuala yote ya kwenye Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa