



Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa anayeshughulikia masuala ya afya .Mhe. dkt.Jafar Raja
b Seif amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwa kutembelea na kukagua utekelezaji na uendeshwaji wa kituo cha afya mtwango kilichojengwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya njombe. Katika ziara hiyo mhe.dkt. Jafar Rajab Seif amefurahishwa na kuvutiwa na utekelezaji wa kituo cha afya mtwango kupitia mapato ya ndani. Aidha mhe. naibu waziri amepitia na kukagua majengo nane (08) : Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ,Jengo la mionzi ( X-RAYS),Jengo la baba ,mama na motto (RCH) ,Jengo la wazazi (METERNITYWORD),Jengo la Wagonjwa waliolazwa( IPDO),Jengo la kuhifadhi maiti (MOCHWARI) na jengo la upasuaji (THEATRE) ambapo kilitumia kiasi cha milioni tsh.927,496 , 886 .34 mpaka kufikia januari2026.Pia Mhe.naibu wa tamisemi anayeshughulikia masuala ya afya amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya njombe,ndugu Christopher sanga na mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya ya njombe,mhe. Israel mhada kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuanza kujenga uzio na nyumba za watumishi ili kuboresha huduma zaidi kwa wananchi .



Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Kidegembye,Barabara ya Lupembe
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa