
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka awaasa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kufanya kazi kwa weledi ya kukusanya taarifa na maoni ya Mahitaji ya Wananchi na kuyafikisha kwa Viongozi ili kufanyiwa utatuzi na kuleta dhana halisi ya Maafisa hao ya kuwa kiunganishi baina ya Serikali na Wananchi.
Hayo ameyasema kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi cha Kitaifa cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali ambacho kimefanyika kwa Siku mbili (2) kuanzia Disemba 17 hadi Disemba 18, 2025 kwenye Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.
Aidha amewataka Maafisa hao kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa zote muhimu kwa wakati kuhusiana na masuala mbali mbali yanayofanywa na serikali ikiwemo utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na mahitaji yao muhimu.
Kikao kazi hicho kimeongozwa na Kaulimbiu ya: “Utu na Mawasiliano Yenye Uwajibikaji” kimeandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu kwa kushirikiana na Idara ya Habari (Maelezo).

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Kidegembye,Barabara ya Lupembe
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa