• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
NJOMBE DISTRICT COUNCIL
NJOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili na Ardhi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Ufugaji Nyuki
    • Kata
    • Vijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Misitu na Upandaji Miti
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Uwezeshaji kwa Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyopendekezwa.
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Tukio
    • Gazeti/Jarida

Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango

Majukumu ya jumla:

Kamati hii inawashirikisha wenyeviti wa Kamati zote za kudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja . Aidha madaraka ya Kamati hii ni kama ya Kamati zingine za kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanya kazi/majukumu ya Kamati zingine za kudumu. Kwa ujumla, majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kwa kupitia vikao vyake.

Majukumu Maalum ya Kamati:

  • Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato.
  • Kuwakilisha mapendekezo ya Bajeti na mpango wa maendeleo kwenye Halmashauri.
  • Kusimamia utunzaji wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na kuomba vibali maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa
  • Kufikiria na, pale inapowezekana, kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu heria Ndogo na utendaji katika ngazi za chini za Halmashauri.
  • Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha(re-allocation) yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeka kwa Halmashauri.
  • Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri
  • Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri
  • Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290.
  • Kupokea na kujadili  taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu  wa Sheria za Serikali za Mitaa.
  • Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmashauri, kwa kuzingatia  taratibu zilizowekwa na Waziri na taratibu nyingine zitakazo wekwa na Halmashauri.
  • Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususan kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vifaa hutumika;
  • Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi,ada na ushuru mbalimbali, vinavyotolewa na Halmashauri.
  • Kufikiria mapendekezo ya Bajeti na Mipango ya Maendeleo ya kila kamati ya kudumu na kuiwasilisha kwenye Halmashauri ili idhini.
  • Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatua stahiki ya kuchukua kuondoa mapungufu katika mapato au ziada matumizi.
  • Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye Halmashauri ili  idhini;
  • Kupokea mahesabu ya mwaka  ya Halmashauri na kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
  • Kupitia na kuidhinisha mpango wa  manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia mpango wa Bajeti uliopitishwa na Halmashauri;
  • Kupitia  taarifa ya kila robo mwaka kuhusu Manunuzi iliyowasilishwa  na Afisa Masuuli;
  • Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa;
  • Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuzi au ukaguzi wa kuduma au vifaa vilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi, itafanyika hivyo endapo itadhihirika kwamba maelezo yaliyotolewa kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma haya ridhishi;
  • Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mujibu wa Sheria husika;
  • Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayowasilishwa kwenye kamati na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;
  • Kupendekeza njia na taratibu za kuondosha vifaa chakavu Uondoaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu;
  • Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo mwaka
  • Kupendekeza kwa Halmashauri hatua za kuchukuwa kuhusu kutafuta madeni ya Halmashauri;
  • Kushughulikia Sera kuhusu kukopa na uwekezaji.
  • Kujadili na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi,ada na ushuru mbalimbali vinavyotozwa na Halmashauri.
  • Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Halmashauri nyingine.
  • Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya  mapato ya vijiji na miji midogo kwa mujibu wa sheria.
  • Kuteua wakaguzi wa fedha/mali za Serikali za vijiji kwa mujibu wa Sheria.
  • Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kuhusu mambo yote yanayohusu masuala ya ajira na kinidhamu ya wafanyakazi na watumishi.
  • Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.
  • Kupokea na kutoa uamuzi juu ya mapendekezo ya watumishi wanao kwenda masomoni.
  • Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo ,nyumba,usafiri,matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.
  • Kupendekeza Sheria Ndogo zinazohusu kamati hii.




Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI YA MUDA February 26, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WA KUANDIKA TAREHE 28-29/12/2020 December 19, 2020
  • TANGAZO MABADILIKO ENEO LA KUFANYIA USAILI December 25, 2020
  • TAARIFA KWA UMMA-TANZIA February 03, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE YAKOMBA MILIONI 20 MSHINDI WA KWANZA USAFI TANZANIA.

    April 08, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA NJOMBE, MHE.JUMA SWEDA AKIOGEA NA WAFANYAKAZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI

    February 07, 2025
  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WAMETEMBELEA NA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    January 30, 2025
  • KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA WILAYA YA NJOMBE(DCC), DC KISSA AUNDA KAMATI MAALUMU KUCHUNGUZA CHANGAMOTO ZA VIWANDA VYA VIWANDA VYA CHAI WILAYA YA NJOMBE

    January 24, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

KAMATI YA SIASA WILAYA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Biashara
  • Huduma za Afya
  • Jarida/Gazeti

Viunganishi Linganifu

  • President's Official Website
  • President's Office,Public Service Management and Good Governance
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • National Bureau of Statistics(NBS)
  • Tanzania Information Services-Maelezo
  • Government Portal

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.

    Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe

    Namba ya Simu: +255 26 2782111

    Simu Kiganjani:

    Barua pepe: ded@njombedc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa