Akifunga Mahafali ya Tano ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ursuline iliyopo Kata ya Ikuna Kijiji cha Nyombo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe , Ndg Christopher Aloyce Sanga amewataka wazazi na walezi wenye watoto wa kuhakikisha wanawapa kipaumbele watoto wa kike katika suala la kuwapatia elimu .
" Nimefurahi kuwaona Wanafunzi wanafanya masomo ya kwa vitendo ni namna gani wameandaliwa vizuri, hapa kwa kweli nawapongeza Wazazi kwa malezi bora waliyowapatia mabinti zao pia nawapongeza walimu wote kwa kuwapa elimu bora ambayo itaenda kuwa mkombozi wa maisha yao kwa baadae " - Ndg. Christopher Aloyce Sanga ( Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe)
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Kidegembye,Barabara ya Lupembe
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa