Naibu waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitala ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mapato ya ndani pamoja na kusaidia kuinua vijana wilayani hapa.
Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea kikundi cha kupasua kokoto cha Hilary Genuine Group kilichopo katika Kata ya Mtwango ambacho kimepewa mkopo wa milioni 20 na Halmashauri ya wilaya ya Njombe ikiwa ni sehemu ya mikopo ya vijana, wanawake na walemavu pamoja na mradi wa ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Itunduma kilichopo Kata ya Mtwango wilayani Njombe.
Akizungumza katika ziara hiyo mbali ya kuipongeza Halmashauri kwa kufanikisha kutoa mkopo kwa kikundi hicho, amewataka wataalamu wa Halmashauri kutoa ushauri wa namna ya kuzipanga kokoto katika madaraja tofauti ili kuongeza soko.
“Zipo Halmashauri hazijapeleka ata shilingi kwenye miradi ya maendeleo wao kazi ni kujilipa posho za safari na semina lakini nyinyi nimeona miradi miwili, ujenzi wa zahanati pamoja na vijana ambapo mmepeleka pesa ya mapato ya ndani nawapongeza sana” alisema Wahitara.
“Nimeona mmetenga bajeti ya milioni 20 kwa ajili ya zahanati hii sasa kuna hela zinaletwa toka serikali kuu milioni 24 mtachanganya na hizo zenu ili muweze kumalizia zahanati hii na wananchi waweze kupata huduma” aliongeza Waitara
Mradi huu hadi kukamilika kwake utatumia zaidi ya milioni 111 ambapo hadi sasa zaidi ya milioni 46 zimekwishatumika ambapo Halmashauri imepeleka jumla ya milioni 10 huku michango mingine ikiwa ni nguvu za wananchi, mfuko wa jimbo pamoja na wadau wa maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi cha Hilary Genius Group , Hilary Shem Mgindo amesema kuwa fedha walizopewa mkopo na Halmashauri zimewasaidia sana katika kuwainua kimaisha.
“Mkopo huu umesaidia kuinua mradi wetu na mafanikio yapo mengi ikiwemo wanakikundi kuweza kununua viwanja na kujenga pamoja na kuboresha maisha yetu” Alisema Mgindo
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa