Waziri wa Afya Nchini Tanzania Jenister Mhagama ameitangaza Halmashauri ya wilaya ya Njombe Kwa upande wa Halmashauri za wilaya kuwa Mshindi wa kwanza kwa usafi kupitia mashindano ya Afya na usafi wa mazingira.
Mhe.Mhagama amesema Halmashauri ya wilaya ya Njombe imekuwa Mfano Tanzania kwa usafi kwani Imeendelea kushika nafasi ya kwanza kila mwaka na kuipa zawadi ya shilingi Milioni 20,000,000 kwa kazi nzuri.
Katika mashindano hayo kwa ngazi za Vijiji,Kijiji Cha Ikuna kimekuwa Kijiji Cha kwa kwanza kwa usafi na kupata ngao na fedha kiasi Cha shilingi 4,000,000, Kijiji Cha kidegembye mshindi wa pili na kupata cheti na fedha kiasi Cha shilingi milioni 2,000,000 huku Shule ya msingi Ikuna ikiwa mshindi wa kwanza kwa ngazi ya shule za msingi na kupata ngao na fedha taslimu shilingi milioni 4.
Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Christopher Sanga ameipongeza timu ya wataalamu wa Afya kwa kazi nzuri anbayo imekuwa ikiiweka Halmashauri yake kwenye ramani bora ya usafi nchini.
Kwa miaka tisa mfululizo Halmashauri ya wilaya ya Njombe Imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yanayochagizwa na ujenzi wa Vyoo Bora,udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa