Halmashauri ya wilaya ya Njombe imeanza ujenzi wa Hospitali katika eneo la Matembwe baada ya kupata fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Tayari Halmashauri imepokea kiasi cha 1,500,000 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali ambayo yatajengwa na mafundi wa kawaida kupitia force account kwa kusimamiwa na wataalam kutoka katika Halmashauri.
Majengo yaliyopendekezwa kuanza ni pamoja na jengo la utawala, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), stoo ya dawa, Maabara, jengo la vipimo vya mionzi(x-ray),jengo la kufulia nguo(Laundry) na jengo la wazazi .
Hadi sasa eneo la mradi limeshasawazishwa kwa ajili ya kuanza kushimba msingi huku baadhi ya maandalizi ya miundombinu muhimu ikiwemo kusogeza maji eneo la ujenzi ambapo wananchi wameshiriki uchimbaji wa mtaro wenye urefu wa kilometa mbili na nusu.
Kazi nyingine zilizofanyika ni pamoja na kujenga stoo ya muda na vyoo, Kutengeneza bango la mradi ,pamoja na Ufungaji wa solar katika banda la kuhifadhia malighafi zitakazotumika kwenye ujenzi yamekamilika.
Katika kufanikisha mradi huo Halmashauri imechangia kiasi cha milioni 20 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali ili kuweza kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo.
Aidha, vifaa kwa ajili ya ujenzi ikiwemo matofali, mawe, mchanga nondo pamoja na saruji zimeshafika eneo la mradi na uchimbaji wa msingi unatarajiwa kuanza muda wowote.
Kuanza kwa ujenzi wa hospitali hii utaboresha huduma za afya katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe kutokana na Halmashauri kutokuwa na hospitali hivyo kutegemea huduma hasa za upasuaji kutoka katika kituo cha afya Lupembe pekee.
Halmashauri ya wilaya ya Njombe ina jumla ya vituo 27 vya kutolea huduma za afya ambapo Vituo vya Afya viko 4 vyote vikiwa ni vya serikali, zahanati ziko 23 ambapo za serikalini zipo 19 na nne ni za mashirika ya dini.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa