A: UTANGULIZI
Taratibu za kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Mfuko wa afya ya jamii ni mfuko wa hiari wa uchangiaji wa gharama za huduma za afya ambazo mteja analipia kabla ya kupata huduma (pre-payment scheme). Uchangiaji wa mfuko huu unatokana na sera ya serikali ya uchangiaji gharama za huduma za afya mwaka 2001(CAP 409) na sheria ndogo ya Halmashauri ilipitishwa na kutanganzwa na gazeti la serikali namba 8.vol 84 la tarehe 21/02/2003.
B: UTARATIBU WA UCHANGIAJI
Wanachama wa mfuko wa afya ya Jamii (CHF)huu huchangia kwa kaya ambapo kila kaya huchangia kiasi cha Tsh 10000/= kwa muda wa mwaka 1 ambapo ada ya uanachama inamuwezesha mkuu wa kaya kutibiwa pamoja na wategemezi wake watono (5) katika kituo cha kutolea huduma alichoandikisha na vituo vingine ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na wategemezi wanaozidi katika kaya hiyo huandikisha kama kaya nyingine.
Kaya ambayo haipo tayari kujiunga hulazimika kulipia gharama ya papo kwa papo kila mgonjwa anapokwenda kupata huduma kiasi cha Tsh 5000/=.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa