• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
NJOMBE DISTRICT COUNCIL
NJOMBE DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Maji
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili na Ardhi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Ufugaji Nyuki
    • Kata
    • Vijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Misitu na Upandaji Miti
    • Sekta ya Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ardhi na Maliasili
    • Uwezeshaji kwa Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyopendekezwa.
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Tukio
    • Gazeti/Jarida

Zaidi ya Bilioni 25 kutekeleza shughuli mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe 2018/2019

Tarehe iliyowekwa: February 7th, 2018

Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Njombe limepitisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 wilayani hapa.

Katika mapendekezo hayo baraza hilo limepitisha kiasi cha zaidi ya bilioni 25.2  kutumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.

Akisoma mpango na rasimu ya  bajeti  kwenye kikao cha baraza la madiwani ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Bi Monica Kwiluhya alivitaja vyanzo vya kufanikisha bajeti hiyo kuwa ni Serikali Kuu, wafadhili, mapato ya ndani, uchangiaji wa huduma za afya, uchangiaji wa ada kidato cha tano na sita pamoja na mchango wa jamii kwenye miradi ya maendeleo.

Akiainisha mchanganuo wa vyanzo hivyo  Bi Kwiluhya alibainisha kuwa Serikali kuu inatarajiwa kuchangia kiasi cha bilioni 20.179, wafadhili bilioni 2.965, mapato ya ndani halisi bilioni 1,439, uchangiaji huduma za afya  zaidi ya milioni 140, uchangiaji ada ya kidato cha tano na sita milioni 42 huku mchango wa jamii kwenye miradi ya maendeleo ukiwa ni kiasi cha milioni 520.

Bi kwiluhya alifafanua kuwa  mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya wilaya ya Njombe imekadiria kutumia zaidi ya bilioni tano ( 5) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri.

“Kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe haina hospitali ya wilaya kutokana na Halmashauri hii kugawanyika katika halmashauri tatu hivyo tumeweka maombi maalumu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali kiasi cha bilioni mbili  ambazo ni fedha za awamu ya kwanza” alisema Bi Kwiluhya.

Aliongeza kuwa katika kufanikisha hilo tayari Halmashauri imetenga bajeti ya milioni 180 kupitia mapato yake ya  ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya wilaya itakayojengwa katika Kata ya Matembwe wilayani Njombe.

Aliyataja maeneo ya kipaumbele kuwa ni miradi ya maendeleo itakayoleta matokeo ya haraka (Quick Wins) ambayo itasaidia kuinua uchumi, kurejesha asilimia 20 ya mapato ya ndani kwenye vijiji, pamoja na kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

Maandalizi ya mpango na bajeti wa Halmashauri ya Wilaya Njombe umeanza katika ngazi za vijiji ambapo jamii imeshiriki katika kuibua miradi na kujadiliwa katika mikutano mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji.

Sambamba na hilo bajeti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia  Utekelezaji wa Malengo Makubwa ya Dira ya Maendeleo ya taifa mwaka 2025, Malengo ya maendeleo endelevu kidunia 2016-2030, Mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/2017-2020/2021 pamoja na muongozo wa uandaaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019.

Miongozo mingine iliyozingatiwa wakati wa uandaaji wa bajeti ni Hotuba ya Rais wa Jamhuri hya Muungano wa Tanzania wakati akilizindua bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20,  Novemba 2015, Mpango mkakati wa Halmashauri wa miaka mitano (2016/2017-2020/2021), mipango shirikishi ya jamii kwa kutumia dhana ya Fursa na vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) pamoja maelekezo  yaliyotolewa katika Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015






Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI YA MUDA February 26, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI WA KUANDIKA TAREHE 28-29/12/2020 December 19, 2020
  • TANGAZO MABADILIKO ENEO LA KUFANYIA USAILI December 25, 2020
  • TAARIFA KWA UMMA-TANZIA February 03, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE YAKOMBA MILIONI 20 MSHINDI WA KWANZA USAFI TANZANIA.

    April 08, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA NJOMBE, MHE.JUMA SWEDA AKIOGEA NA WAFANYAKAZI WA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI

    February 07, 2025
  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WAMETEMBELEA NA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    January 30, 2025
  • KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA WILAYA YA NJOMBE(DCC), DC KISSA AUNDA KAMATI MAALUMU KUCHUNGUZA CHANGAMOTO ZA VIWANDA VYA VIWANDA VYA CHAI WILAYA YA NJOMBE

    January 24, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

KAMATI YA SIASA WILAYA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Biashara
  • Huduma za Afya
  • Jarida/Gazeti

Viunganishi Linganifu

  • President's Official Website
  • President's Office,Public Service Management and Good Governance
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • National Bureau of Statistics(NBS)
  • Tanzania Information Services-Maelezo
  • Government Portal

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.

    Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe

    Namba ya Simu: +255 26 2782111

    Simu Kiganjani:

    Barua pepe: ded@njombedc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma Zetu

Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa