Jumla ya wanafunzi 926 wanafanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne kwa mwaka 2018 katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Mtihani huu ambao umeanza Novemba 5 na kumalizika Novemba 23 mwaka huu, umewajumuisha watahiniwa wavulana 311 na wasichana 615 kutoka shule 12 katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Kati ya shule 12 Zinazofanya mtihani huu 10 ni za serikali na mbili ni binafsi. Katika watahiniwa 926 wanaofanya mitihani , watahiniwa kutoka shule za serikali wako 818 na watahiniwa 108 wanatoka katika shule za binafsi.
Shule za Sekondari zinazofanya mitihani hii upande wa shule za serikali ni Idamba, Ikuna, Itipingi, J.M Makweta, Kidegembye, Lupembe, Manyunyu, Sovi, Mulunga na Ninga huku shule za binafsi zikiwa ni Collegine Girls pamoja na Mtwango.
Aidha, watahiniwa binafsi wako 37, wasichana wakiwa ni 15 na wavulana 22 ambao watafanya mitihani katika vituo viwili ambavyo viko katika shule ya Sekondari Mtwango na Lupembe.
Halmashauri tayari imefanya maandalizi yote muhimu ikiwemo upelekaji wa mitihani na nyaraka mbalimbali katika vituo na maeneo ambayo mitihani itafanyika..
sambamba na hili Halmashauri inapenda kutoa kwa wazazi na walezi wa wanafunzi kuhakikisha wanawapatia watoto wao mahitaji muhimu yatakayowawezesha kufanya mtihani katika hali ya utulivu. Upande wa wanafunzi wanatakiwa kufanya mtihani katika hali ya utulivu na kujiepusha na vitendo vyovyote vya udanganyifu ambavyo vitapelekea kufutiwa mitihani yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa