Jumla ya watahiniwa 802 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa mwaka huu 2017.
Katika mtihani huu unaofanyika kuanzia Leo Octoba 30 hadi Novemba 11 mwaka huu, watahiniwa Wavulana wako 277 na wasichana 525. Upande wa watahiniwa wa kujitegemea wako 46 ikiwa wavulana wako 20 na wasichana 26 kutoka katika shule 12 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Watahiniwa wanaofanya mtihani wa maarifa (Qualifying Test) wako wawili (2) ikiwa msichana ni mmoja na mvulana mmoja.
Jumla ya shule 12 zinatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne huku shule 10 zikiwa ni za Serikali na shule mbili (2) za binafsi.
Shule zinazotarajiwa kufanya mtihani upande wa shule za Serikali ni Idamba, Ikuna, Itipingi, J.M Makweta, Kidegembye, Lupembe, Manyunyu, Sovi, Mulunga na Ninga huku shule za binafsi zikiwa ni Collegine Girls pamoja na Mtwango.
Upande wa wasimamizi watakaosimamia mtihani huu wako 47 wakiwemo wasimamizi wakuu 12, wasimamizi wa nje 23 pamoja na walimu wakuu 12.
Adha, maandalizi ya mtihani huu yamekamilika ikiwemo vifaa vyote muhimu kufika kwa wakati kwenye vituo vya kufanyia mitihani.
Halmashauri inapenda kutoa wito kwa wazazi na walezi wa wanafunzi kuhakikisha wanawapatia watoto wao mahitaji muhimu yatakayowawezesha kufanya mtihani katika hali ya utulivu. Upande wa wanafunzi wanatakiwa kufanya mtihani katika hali ya utulivu na kujiepusha na vitendo vyovyote vya udanganyifu ambavyo vitapelekea kufutiwa mitihani yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa