Jumla ya wanafunzi 2278 wa darasa la saba wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Mtihani huo ambao utafanyika kwa siku mbili kote nchini kuanzia Septemba 5 hadi 6 unahusisha wasichana 1246 na wavulana 1032 kutoka katika shule 53 zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
wasimamizi 165 wanatarajiwa kusimamia ufanyikaji wa mtihani huo huku kiwango cha ufaulu kikitarajiwa kuwa zaidi ya asilimia 80.
Maandalizi yote muhimu kwa ajili ya ufanyikaji wa mitihani hiyo yamekamilika ikiwemo upelekeji wa mitihani katika vituo 11 teule vya kuhifadhia mitihani.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inapenda kutoa wito kwa wazazi, na walezi wa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani kuhakikisha wanawapatia watoto wao mahitaji muhimu yatakayowawezesha kufanya mtihani katika hali ya utulivu.
Wanafunzi wote wanatakiwa kutojiusisha na mbinu zozote zile za udanganyifu wakati wa kufanya mtihani ambazo zitapelekea kufutiwa matokeo yao.
Halmashauri ya wilaya ya Njombe inajumla ya shule 53 za msingi huku shule za Serikali zikiwa 52 na binafsi moja.
Katika mtihani uliofanyika Mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 2268 kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ambapo wavulana walikuwa 950 na wasichana 1318
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa