Katika kuhakikisha wakulima na wafugaji wanakuwa na soko la uhakika la kuuza bidhaa na mifugo yao Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imeanzisha mnada wa mifugo katika Kijiji cha Ilunda Kilichopo katika kata ya Mtwango wilayani Hapa.
Kuanzishwa kwa mnada huu amboa utakuwa ukifanyika kila tarehe 12 ya kila mwezi kutawawezesha wafugaji kuuza mifugo yao pamoja na wanunuzi kupata sehemu ya uhakika ya kununua mifugo kwa ajili ya ufugaji na lishe.
Mnada huu ni moja ya mikakati ya Halmashauri ya kuwainua wananchi wake kiuchumi kwa kuwawekea mazingira bora ya kuuza na kununua bidhaa mbalimbali.
Toka kuanzishwa kwa mnada huu mwitikio umekuwa mzuri ambapo wananchi mbalimbali wamekuwa wakiuza bidhaa ikiwemo mbogamboga na matunda huku kivutio kikubwa kikiwa ni nyama ya mbuzi ambayo imekuwa ikichomwa kwa ustadi wa hali ya juu na watu wa jamii ya wamasai kutoka Mbalili Mkoani Mbeya ambapo kila siku ya mnada huwa wanashiriki.
Upande wa mifugo ambayo imekuwa ikiletwa kwa ajili ya kuuzawa ni apamoja na ng’ombe, mbuzi pamoja na kuku.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imeweka mikakati madhubuti katika kuboresha mnada huo na kuufanya kuwa mnada mkubwa katika mkoa wa Njombe. Tayari Halmashauri imeshaboresha vitu vya muhimu ikiwemo miundombinu ya choo na maji ya uhakika.
Halmashauri ya wilaya ya njombe inatoa wito kwa wananchi wote kutembelea katika mnada wa Ilunda ili kuweza kujipatia kitoweopamoja na kujifunza mambo mbalmbali kutoka kwa wakulima na wafugaji kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Njombe, mbeya na Iringa.
Aidha wakulima na wafugaji wanashauriwa kupeleka mifugo na bidhaa zao katika mnada wa Ilunda kila tarehe 12 ya kila mwezi kwa kuwa ni sehemu ya uhakika ya kuuza mifugo na bidhaa zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa