Kijiji cha Ikondo kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kipo umbali wa kilometa 90 kutoka makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya. Kijiji hiki kinachopatikana katika kata ya Ikondo,Tarafa ya Lupembe kina watu 4,025 kati yao wanawake ni 2,228 na wanaume ni 1,797
Mwaka 2018 kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kijiji hiki kilipewa fursa ya kuibua miradi mitatu ya miundombinu.
Kupiti fursa hiyo kilichagua ujenzi wa madarasa 5, matundu 12 ya vyoo ofisi moja ya walimu pamoja na nyumba mbili za walimu (Two in one) zimejengwa kwa awamu na zinagharimu kiasi cha 215,627,896.80
Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo umegharimu kiasi cha 72,041,202.36, Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 2,Ofisi moja ya walimu na matundu 6 ya vyoo huku mradi wa ujenzi wa nyumba 2 (two in one) za walimu na vyoo ukigharimu zaidi ya milioni 71.
Madarasa yanayojengwa yanahusisha madawati na fenicha nyingine muhimu kwa ajili ya wanafunzi kuwa na mazingira bora ya kujifunzia pamoja na walimu kufundisha.
Kutokana na uhitaji mkubwa wa shule wananchi wa walipangiana zamu katika kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuchimba msingi, kuleta mawe pamoja na kufyatua tofali.
Kwa sasa ujenzi umepamba moto ambapo tayari madarasa matatu pamoja na vyoo 6 vimekamilika huku madarasa yaliyobaki yako katika hatua za ukamilishaji na mwezi Februari wanafunzi wataanza kusoma.
Mbali na kupata faida ya kujengewa shule na TASAF, kijiji cha ikondo kina wanufaika Jumla ya kaya za walengwa 202 zimehawilishiwa fedha kiasi cha shilingi 109,948,000.00 kwa awamu 20 za malipo.
Fedha hizo zimewawezesha kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na kufuga na kujiongezea kipato.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa