Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imepokea jumla ya vitabu 5,935 kutoka katika mradi wa vitabu vya watoto Tanzania ambao unafadhiliwa na shirika la UNICEF.
Vitabu vilivyopokelewa ambavyo ni vya kujifunzia na kufundishia ni kwa ajili ya darasa la kwanza na la pili na vitagawanywa katika shule 52 za msingi zilizoko katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Darasa la kwanza vitabu vilivyopokelewa ni 3,636 huku darasa la pili vikiwa ni 2,299 na hivyo kuongeza idadi ya vitabu jambo ambalo litachochea na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Ugawaji wa vitabu ni miongoni mwa mikakati ya serikali ambayo inakwenda sambamba na utoaji wa elimu bure ili kuweza kukidhi mahitaji kutokana na muitikio mkubwa wa wazazi katika kupeleka watoto shule.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali inaendelea na jitihada za kuboresha mazingira ya Shule za Msingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu pamoja na vyoo vya kisasa ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya shule za msingi zinavyoo vya kisasa ambavyo vinazingatia mahitaji maalumu kwa wasichana na walemavu.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa