Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Samwel Sweda leo tarehe 07/9/2025 amefanya kikao maalumu na Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe chenye malengo ya kusikiliza kero na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa kupitia fedha za Mapato ya ndani na Fedha kutoka Serikali kuu.
Aidha Mhe. Sweda amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kuweza kuifahamu miradi yao wanayoisimamia na kutumia fedha vizuri kwenye Miradi. “ Wakuu wa Idara na Vitengo nawaomba sana twendeni tukatembelee na kusimamia miradi ya idara yako , maana nitafanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ,hvyo sitotaka kusikia wala kuona mradi haujamilika na fedha zimeisha hvyo sitowaelewa kabisa kuhusu hilo.
Pia Mkuu wa Wilaya alisikiliza kero za Watumishi wa ngazi za chini ,ambapo alipokea kero za Watumishi ambayo ni kufanyakazi masaa ya ziada pasipo malipo na kumuagiza afisa utumishi kuzishughulikia mara moja ili watumishi waweze kupata haki zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa