Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amepiga marufuku wanafunzi wa Shule za Sekondari wilayani Njombe kukaa kwenye nyumba za kupanga maarufu kama jina la gheto.
Akizungumza katika baraza maalumu la madiwani la kujadili taarifa na mpango kazi wa hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 katika Halmashauri ya Wilaya Njombe, Ole sendeka alisema ni marufuku kwa wazazi kuwapangia watoto wao vyumba katika nyumba zilizo karibu na shule na kuwaagiza madiwani kufuatilia na kufikisha taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri kwa wazazi wanaokaidi agizo hilo.
“Watoto wa shule wanaokwenda kupangishiwa vyumba vya kupanga “magheto” na wanakuwa wanatoka hapo kwenda shule hilo napiga marufuku na sio sahihi, ni jukumu letu sisi kufuatilia, msaidieni Mkuu wa Wilaya kwa kumfikishia taarifa ili aweze kuchukua hatua sahihi.”Alisema Ole Sendeka
Ole sendeka aliongeza kuwa Mkoa wa Njombe una neema ya hali nzuri ya hewa, vitega uchumi, na vyakula vingi hivyo viongozi wa Kata husika wahakikishe watoto wote wa Shule za Msingi na Sekondari wanapata chakula cha mchana shuleni.
Aliwataka madiwani kushirikiana na wazazi katika maeneo yao kuweka mikakati ya kujenga mabweni ili wanafunzi wawe katika hali ya usalama na kuweka mkazo kwenye masomo jambo litakaloongeza ufaulu.
Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Njombe amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri kufuatilia watumishi wenye vyeti feki na mishahara hewa ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Nimemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe aniletee orodha ya watumishi na watu wengine waliochukua fedha za serikali pasipo kustahili ili wachukuliwe hatua stahiki” Alisisitiza Ole Sendeka
Aidha, Aliziagiza Halmashauri kuhakikisha zinafuatilia madeni ya SACCOS ili yarejeshwe kwa wakati huku akizitaka Halmashauri kupeleka asilimia 20 ya fedha vijijini kwa wakati na asilimia 10 ambazo 5 za mfuko wa maendeleo ya vijana na 5 za mfuko wa maendeleo ya wanawake.
“Fedha hizo lazima zipelekwe kwa wakati ili kusaidia maendeleo katika maeneo ya msingi lakini lazima kuanza kufuatilia vyama vya ushirika na SACCOS jinsi vinavyoji
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa