Jimbo la Lupembe, leo Januari 05,2024 limeendesha Mafunzo kwa Watendaji wa Uandikishaji wa ngazi ya Kata (ARO KATA) kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Maafisa Watendaji wa Uandikishaji ngazi ya Jimbo na kuhudhuriwa na Maafisa ngazi ya Mkoa na kutoka Tume huru ya Uchaguzi..
Akifungua mafunzo hayo Afisa mwandikishaji wa Jimbo la Lupembe, Mkoa wa Njombe Ndugu Cassian Nkunga amewataka Watendaji hao kufanyakazi kwa umakini na weledi ili kuhakikisha Wananchi
wote wanaotakiwa kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura wanafikiwa.
Awali Watendaji hao waliweza kupatiwa Kiapo cha utii na kutunza siri kilichotolewa na Ndugu Godfrey Msemwa, Hakimu wa Mahakama ya Lupembe.
Jumla ya Watendaji wa Uboreshaji 12 kutoka Kata 12 za Jimbo la Lupembe lenye jumla ya vijiji 45 na Vitongoji 227 wanapatiwa Mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa muda wa Siku Mbili (2) Tarehe 5-6/01/2025
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa