Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Njombe limeipongeza Halmashauri kwa kuweza kupata hati safi katika hesabu za serikali za mwaka wa fedha 2017/2018.
Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Valentino Hongoli wakati akisoma hotuba yake kwenye ufunguzi wa baraza la kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Hongoli aliipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi katika hesabu za jumla, miradi ya maendeleo ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) miradi ya maji pamoja na mfuko wa pamoja wa Afya (busket fund)
“ Nikupongeze Mkurugenzi mtendaji na timu yako kwa kazi nzuri mliyofanya hadi kuweza kupata hati safi, mafanikio haya hayajaja kama ndondokela au ngekewa bali ni kutokana na ushirikiano uliopo baina ya waheshimiwa madiwani, wataalam na viongozi mbalimbali wa serikali. Naomba ushirikiano huu uendelee na tuendelee kufanya vizuri katika sekta mtambuka” alisema Hongoli.
Aidha, aliipongeza Halmashauri ya wilaya ya Njombe kuweza kukusanya kwa asilimia 82 mapato ya ndani kuanzia mwezi Julai hadi machi mwaka wa fedha 2018/2019
“ Kasi tunayokwenda nayo naamini tutavuka malengo na niwapongeze kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato, lakini isiwe kukusanya tu na matumizi yake yasimamiwe vizuri katika kutekeleza miradi ya maendeleo” Alisema Hongoli.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Njombe limefanyaka siku mbili kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Siku ya kwanza madiwani walipata wasaa wa kuwasilisha utekelezaji wa taarifa kwenye Kata na siku ya pili utekelezaji wa shughuli za Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa