Katika kuboresha huduma za afya wilayani Njombe kituo cha afya cha Lupembe kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kimeanza huduma ya upasuaji kwa wakinamama wajawazito katika Kata hiyo.
Kuanza kutolewa kwa huduma hiyo ni ukombozi kwa wananchi wa Kata ya Lupembe pamoja na Tarafa ya Lupembe na kutasaidia kuzuia na kupunguza vifo vya kinamama na watoto kutokana na kutokuwepo kwa huduma hiyo katika maeneo hayo.
Tangu huduma ya upasuaji wa kinamama wajawazito kuanza kutolewa katika kituo cha afya Lupembe jumla ya wakinamama wajawazito 13 tayari wamefanyiwa upasuaji na wote wanaendela vizuri.
Hadi kukamilika kwake wodi ya upasuaji imegharimu zaidi ya Milioni 26 na Halmashauri kwa sasa imejikita katika kukamilisha wodi ya kinamama na watoto katika kituo hicho.
Akizungumzia mafanikio hayo katika sekta ya afya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi Monica Kwiluhya alisema kwa sasa Halmashauri imejikita kuhakikisha inakamilisha jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Lupembe.
“Tumefanikiwa kuanzisha huduma ya upasuaji katika kituo cha Afya Lupembe sasa tumejikita kutafuta jenereta ili huduma ya upasuaji ifanyike kwa ufanisi lakini tutakamilisha jengo la mama na mtoto hivi karibuni” alisema Bi Kwiluhya
Aidha, Halmashauri ya wilaya ya njombe kwa sasa imeweka kwenye bajeti kwa ajili ya kujenga chumba cha upasuaji katika kituo cha afya Kichiwa ili kuboresha sekta ya afya wilayani hapa.
Halmashauri ya wilaya ya Njombe inajumla ya vituo vya afya 4 pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya 23 na kituo cha afya Lupembe kinakuwa kituo cha kwanza kutoa huduma ya upasuaji.
Sambamba na kutenga bajeti ya kujenga hospitali ya wilaya Halmashauri inaendelea na ukamilishaji wa vituo vya kutolea huduma katika kila kijiji wilayani hapa.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inajumla ya kata 12 na vijiji 45.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa