Changamoto ya kutowalipa wakulima na wafanyakazi wa sekta ya chai mkoani Njombe imetajwa kusababisha baadhi ya wakulima kutelekeza mashamba ya chai na kujikita kupanda mazao mengine.
Baadhi ya viwanda hivi sasa vinaonekana kutofanya kazi na vingine kushindwa kuwalipa wakulima na wafanyakazi wao hatua iliyochagiza wakulima kukiona Kilimo Cha chai mwiba mkali.
Migomo ya wafanyakazi kwenye viwanda vya chai mkoani Njombe imekuwa ya mara kwa mara ikisababishwa na kucheleweshewa Mishahara yao na kusababisha serikali kuingia lawamani.
Katika Kikao Cha Ushauri wilaya ya Njombe DCC kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa , Baadhi ya wadau wa chai na wakulima wamevitupia lawama viwanda na wawekezaji wa chai huku wakitaka hatua za maksudi Kuchukuliwa ili kunusuru adha kwa wakulima na wafanyakazi.
Baadhi yao ni Mzee Lukule Mponji,Yotham Mhiche,Ally Mhagama na Mchungaji Nelson Godiwe wameishauri na kuitaka Serikali kuendelea kulifanyia kazi changamoto zinazowakuta wakulima na kupelekea kupotea kwa thamani ya zao la chai.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Swalle amemuunga mkono Mhe. Kissa kuundwa kwa Tume itakayochunguza mkwamo wa viwanda vya Chai Njombe ili kupata suluhu ya Kudumu ili kunusuru sekta hiyo.
Theofhord Ndunguru mkurugenzi mkuu Wakala wa Maendeleo ya wakulima wadogo wa Chai nchini anasema Kuporomoka kwa soko la zao Hilo duniani kutokana na kushuka kwa unywaji wa chai kuliko uzalishaji Na hivyo kumesababisha adha kubwa kiuchumi jambo linalosabisha wakulima na wafanyakazi Wengi kulalamika.
Ndunguru amesema viwanda vingi vya chai duniani vikiwemo vya Kenya Uganda na Tanzania vimefungwa kutokana na hasara kubwa ya uendeshaji.
Naye Jaherson Moturi ni mkurugenzi wa viwanda vya Chai vya Kampuni ya DL Group ambaye amekiri kuchelewesha malipo ya wafanyakazi na kwa kiwanda Cha kibena wanadaiwa Mishahara ya Mwezi Mmoja Ambayo Wanatarajia kuilipa hivi karibuni na Ikanga Lupembe miezi miwili.
Kutokana na changamoto hizo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amelazimika kuunda Kamati maalumu ya uchunguzi itakayofanya kazi ya kufuatilia changamoto za viwanda vya chai ili ije na majibu sahihi yatakayowasaidia wakulima na wafanyakazi kupata Fedha zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa