Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Makao Makuu Mhe. Asinaa A. Omari amewaasa Watendaji wa Uandikishaji ngazi ya Kata (ARO KATA) kuhakikisha wanatekeleza vyema majukumu yao wakati wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura ikiwemo kuhakikisha Wananchi wanahudumiwa vyema, usimamizi wa Watendaji watakaokuwa wanatekeleza zoezi la uandikishaji yaani Waandishi Wasaidizi na Waendesha Mashine za BVR pamoja na utunzaji wa vifaa.
Hayo ameyasema leo alipotembelea Jimbo la Lupembe, Mkoa wa Njombe kujionea namna Mafunzo hayo yanavyotolewa na
Maafisa Watendaji wa Uandikishaji ngazi ya Jimbo pamoja na Maafisa kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha amewataka Watendaji hao kuhakikisha Wananchi wote wenye sifa za kuandikishwa kwenye maeneo yao Wanaandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Jumla ya Watendaji wa Uboreshaji 12 kutoka Kata 12 za Jimbo la Lupembe lenye jumla ya vijiji 45 na Vitongoji 227 wamepatiwa Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa muda wa Siku Mbili (2) kuanzia tarehe 05/01/2025 hadi tarehe 6/01/2025.
Kaulimbiu ya Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni "Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora "
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa