Mbali na kuwa na sifa katika utunzaji wa mazingira ambao unakwenda sambamba na upandaji wa miti na kuifanya wilaya hii kuwa ya kijani, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inasifika kwa kuwa kinara katika utekelezaji wa kampeni ya afya na usafi wa mazingira nchin Tanzania.
Haikuwa lahisi kwa Halmashauri hii kuweza kufikia mafaniko haya bali imetokana na umoja na mshikamano uliopo baina ya viongozi kuanzia wale wa chama na serikali. Ilikuwaje hadi Halmashauri hii ikafanikiwa kuwa kinara katika utekelezaji.
Kampeni ya Kitaifa ya afya na usafi wa mazingira nchini Tanzania ilizinduliwa na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete mwaka , 2012 mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Kampeni hii ililenga kuinua kiwango cha upatikanaji wa huduma bora za usafi wa mazingira kwa kuinua uwiano wa kaya zenye vyoo bora kwa zaidi ya asilimia 50% hadi hadi kufikia mwaka 2015.
Sambamba na kuinua kiwango cha upatikananji wa huduma bora za usadi wa mazingira pia ililenga kupunguza kuenea kwa magonjwa yasababishwayo na mazingira machafu (Sanitation related diseases).
Awamu ya kwanza imetekelezwa katika ngazi ya kaya na katika shule za msingi na ililenga kuhakikisha kuwa kila kaya katika eneo la kampeni inakuwa na vyoo bora pamoja na miundombinu ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni.
Ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kampeni hii inatekelezwa katika Kata zote 12, vijiji 45 na vitongoji 227. Aidha, kampeni hii inatekelezwa katika shule 53 za msingi za serikali zilizoko katika Halmashauri.
Katika ngazi ya jamii na kaya mambo mbalimbali yamefanyika ili kuweza kufanikisha kampeni ikiwemo kutoa mafunzo kwa viongozi wa Halmashauri (Wajumbe wa baraza la ushauri la wilaya (DCC), Baraza la madiwani, wakuu wa Idara na vitengo pamoja na wadau mbalimbali waliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Aidha, mafunzo kwa timu ya usimamizi wa kampeni ngazi ya Wilaya ikijumuisha wataalam kutoka idara ya Afya, maji, elimu msingi na Maendeleo ya Jamii yametolewa ili kuweza kufanikisha malengo ya kampeni na kuwa na jamii yenye afya bora kutokana na kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu.
Ili kuweza kufanikisha kampeni ,Halmashauri ilitoa mafunzo ya utekelezaji wa kampeni kwa viongozi wa kata,vijiji na vitongoji vyote pamoja na wahudumu wa afya katika vijiji vyote vya kampeni pamoja na kukusanya takwimu za usafi wa mazingira na kuziingiza katika rejista maalum za kitongoji.
Sambamba na hilo mikutano ya uhamasishaji (uchefuaji) ilifanyika katika vitongoji vyote 227 vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Kutokana na kampeni hii kuhusisha Nyanja mbalimbali mafunzo yalitolewa kwa mafundi ujenzi juu ya ujenzi wa vyoo bora ili kuhakikisha ujenzi wa vyoo unazingatia kanuni zote za afya na usafi wa mazingira.
Baada ya kamapeni na ufuatiliaji wa mara kwa mara unafanyika ili kuona maendeleo ya utekelezaji wa kampeni pamoja na kufanya vikao mbalimbali vya tathmini ya utekelezaji na kubadilishana uzoefu kati ya viongozi wa vitongoji, vijiji, kata, Wilaya na wadau mbalimbali wa usafi wa mazingira katika Halmashauri jambo lililochangia mafanikio makubwa kwenye usafi.
Hali hii imepelekea Halmashauri ya wilaya ya Njombe kuwa kinara kwenye utekelezaji wa kampeni ya afya na usafi wa mazingira nchini Tanzania na kuwa miongoni mwa Halmashauri za mafano kwa kuwa na vyoo bora kuanzia ngazi za Kaya, vijiji na Kata.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa