Katika kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inatekelezeka kwa wakati na kuongeza mapato ya Halmashauri, Halmshauri ya wilaya ya njombe imenunua mtambo mkubwa wa kufyatua tofali.
Mtambo huo ambao unafungwa eneo la uwekezaji lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya njombe unauwezo wa kufyatua tofali 3000 kwa siku zenye kipenyo cha nchi 5 na 6 pamoja na tofali za kutembelea
Uwezo wa mtambo huo utatatua changamoto ya uhaba wa tofali za udongo hasa kipindi cha masika ambapo Halmashauri ya wilaya ya Njombe mvua hunyesha kwa kiwango kikubwa.
Sambamba na kutumia mtambo huu kwa ajili ya kutekeleza miradi , Halmashauri inakusudia kuufanya kama chanzo cha mapato yatakayosaidia kutekeleza shughuli mbalimbali.
Katika kuboresha mapato Halmashauri pia imeanzisha soko la kisasa katika eneo la mtwango ambao litasaidia katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kuwalahisishia wananchi maeneo ya kuanika mbao.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa