Halmashauri ya wilaya ya Wilaya ya Njombe imefanikiwa kutoa mshindi wa kwanza Mkoa wa Njombe na mshindi wa pili Kikanda katika kundi la wafugaji wa N'gombe wa maziwa na samaki kwenye maonyesho ya nane nane mwaka 2019.
Katika maonyesho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa waziri mkuu mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambapo Bi Raheli Mhema kutoka katika Kijiji cha Ikando kilichopo kwenye Kata ya Kichiwa Halmashauri ya wilaya ya Njombe amefanikiwa kushinda nafasi ya kwanza mkoa wa Njombe na nafasi ya pili Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza baada ya kushinda Bi Mhema alieleza kuwa alianza shughuli ya ufugaji mwaka 2013 baada ya kupewa Ng’ombe wa maziwa na Halmashauri ya wilaya ya Njombe kupitia mpango wa maendeleo ya kilimo (DADPs)
Alisema kuwa mwaka 2015 alikwenda Mbeya kwenye maonyesho kwa ajili ya kujifunza zaidi masuala ya ufugaji bora na wakisasa ambapo aliboresha banda pamoja na malisho ya Ng’ombe.
“ Baada ya kupewa elimu kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri ya Njombe nilianza ufugaji ambapo kwa sasa nina Ng’ombe wanne wadogo wako wawili na wakubwa wawili” alieleza Bi Mhema
Aliongeza kuwa sasa ana ng’ombe wake ambaye anauwezo wa kuzalisha maziwa lita 30 kwa siku ambapo asubuhi anatoa lita 17 na jioni 13 na kumpatia zaidi ya 780 kwa mwezi na milioni 9 kwa mwaka baada ya kuondoa gharama za uendeshaji.
“ Upande wa ufugaji ukitoa gharama za uzalishaji ninapata zaidi ya milioni tisa na kilimo Napata zaidi ya milioni 6 nikitoa gharama za uendeshaji hivyo nakusanya zaidi ya milioni 15 kupitia kilimo na ufugaji” alibainisha Bi Mhema.
Kuhusu soko la maziwa Bi Mwenda alisema kuwa anauza maziwa yake katika kiwanda cha Njombe Milk Factory kilichopo Njombe mjini na kuwa na uhakika wa soko.
Akizungumzia kuhusu mafanikio aliyoyapata kupitia ufugaji Bi Mhema alisema kuwa ameweza kujenga nyumba nzuri, kununua usafiri pamoja na kusomesha watoto.
“Mtoto wangu wangu wa Kwanza amemaliza chuo cha uuguzi na mwingine yupo kidato cha tano, fedha zingine nanunulia mashamba na kuwekeza kwenye kilimo” alisema Bi Mhema
Ametoa wito kwa jamii kujikita katika kilimo na ufugaji wenye tija na kisasa ili kuinua kipato cha taifa na familia kwa ujumla.
Maonyesho ya nane nane yamefanyika Mkoani Mbeya ambapo yamehusisha Mikoa ya Nyanda za Juu kusini ikiwemo Njombe, Ruvuma, Iringa, Mbeya, Songwe Rukwa huku yakiwa na kauli mbiu inayosema Kilimo, mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi".
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa