Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ameipongeza halmashauri ya wilaya Njombe kupata hati safi kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.
Ole Sendeka ametoa pongezi hizo wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya , lililoketi kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Akizungumza katika baraza hilo amewapongeza madiwani pamoja na wataalum kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu katika kuendesha halamshauri jambo lililopelekea kupata hai safi.
“ kupata hati safi sio mchezo naomba muendelee kuwa na ushirikiano huo huo ili kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi” alisema Ole Sendeka
“Naomba msiwe mabingwa wa kujibu hoja bali muwe mabingwa wa kuzuia hoja, nimelidhika sana na wapongezeni kwa ubunifu mnaoendelea nao” aliongeza Ole Sendeka
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya njombe, Valentino Hongoli alimuhakikishia mkuu wa mkoa wa njombe halmashauri yake kuendelea kupata hati safi na kuahidi kutekeleza kwa wakati hoja zote zilizotolewa na mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali.
“Mh mkuu wa mkoa kwa niaba ya madiwani na wataalam nakuhakikishia tutaendelea kupata haki safi na maelekezo yako yote tutayafanyia kazi” Alisema Hongoli.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa