Halmashauri ya wilaya ya Njombe imeshika nafasi ya Kwanza Kitaifa katika usafi wa mazingira upande wa Halmashauri za Wilaya nchini na kupeta zawadi ya
shilingi Milioni 50, Kombe pamoja na Cheti.
Zawadi hizo zimetolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa afya mazingira na usafi uliofanyika Jijini Dodoma uliokuwa na kauli mbiu inayosema imarisha
huduma za afya mazingira na usafi katika Mapambano na UVIKO 19 huku Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mhe,
Doroth Gwajima.
Aidha, katika vijiji vitatu vilivyofanya vizuri kitaifa Halmashauri imetoa vijiji viwili vya Itambo kilichopo Kata ya Mfriga ambapo kimeshika nafasi ya Kwanza Kitaifa na kupewa zawadi ya pesa shilingi Milioni 5, kombe pamoja na cheti huku kijiji cha Havanga kilichopo Kata ya Kidegembye kikishika nafasi ya pili kitaifa na kupata zawadi ya shilingi milioni 3 pamoja na cheti.
Sambamba na hilo Shule ya Msingi Iditima Kata ya Mfriga,imeshika nafasi ya pili kwa usafi wa mazingira upande wa shule za msingi na kupata zawadi ya
shilingi milioni 3 na cheti.
kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo Halmashauri ya wilaya ya Njombe imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano ya Usafi wa mazingira na kufanikiwa upata zawadi ikiwemo magari mawili pamoja na fedha.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa