Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Njombe limepitisha rasimu ya mpango na bajeti yenye kiasi cha Bilioni 27.4 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali katika mwaka wa fedha 2019/2020.
Katika rasimu hiyo ya bajeti kiasi cha bilioni 20.7 ni ruzuku ya mishahara, ruzuku ya matumizi mengineyo ikiwa ni bilioni 1.084 , ruzuku ya miradi ya maendeleo ikiwa ni bilioni 3.1 huku mapato ya ndani ikiwa ni bilioni 1. 5 ambayo ni mapato halisi, milioni 465 ni mapato maalum na mchango wa jamii ni milioni 523.
Aidha, Halmashauri ya wilaya ya Njombe inatarajia kutumia kiasi cha Bilioni 3.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri.
Katika fedha hizo zaidi ya milioni 609 ni mchango wa Halmashauri wa asilimia 40 ya mapato halisi ya ndani, Bilioni 2.4 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu na kiasi cha milioni 699 ni fedha za wafadhili.
Akiwasilisha bajeti katika baraza maalum la madiwani , Afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Anganile Daniel alisema kuwa bajeti ya mwaka 2019/2020 imeongezeka kwa asilimia 18 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2018/2019 ambayo ilikuwa ni Bilioni 22.5
“Mheshimiwa mwenyekiti ongezeko la bajeti limetokana na kuongezeka kwa makisio ya vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na bajeti ya mishahara ambayo imeongezeka kutoka bilioni 15.7 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia bilioni 20.7 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 24” alisema Daniel
“Upande wa makisio ya mapato halisi ya ndani yameongezeka kutoka bilioni 1. 4 kwa mwaka 2018/2019 hadi kufikia bilioni 1.5 kwa mwaka wa fedha 2019/2020” alifafanua Daniel
Daniel alibainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya wilaya ya Njombe imewasilisha maandiko ya maombi maalum ya miradi ya kutoa huduma yenye thamani zaidi ya bilioni 15 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kuandaa maandiko ya miradi ya kutoa huduma kwa jamii.
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na Ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati 6 za Upami, Itunduma, Welela, Havanga, Igombola, Lima, kituo cha Afya Ikuna na jengo la mama na mtoto (RCH) katika zahanati ya Mfriga.
Miradi mingine ni ujenzi wa vyoo bora katika vituo 21 vya kutolea huduma za afya, ujenzi wa Miradi ya maji katika vijiji vya Kanikelele, Ikang’asi na Ikuna, ujenzi wa vyumba 52 vya madarasa ya shule za msingi pamoja na ujenzi wa nyumba 10 za walimu wa shule 10 za msingi (two in one)
Sambamba na hilo upo Ujenzi wa mabweni 2 katika shule ya msingi Matembwe, Ujenzi wa matundu 157 ya vyoo katika shule 6 za Sekondari, Ujenzi wa nyumba 249 za walimu wa shule 11 za Sekondari (two in one)
Kuhusu miradi ya kimkakati, Daniel alieleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imewasilisha TAMISEMI andiko la mradi wa ujenzi wa jengo la kibiashara ambalo linatarajiwa kujengwa katika eneo lililopo pembezoni mwa zilipo ofisi za makao makuu ya Halmashauri.
Halmashauri ya wilaya ya Njombe inakata 12 zenye vijiji 45.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa