Katika kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye shughuli mbalimbali za Halmashauri, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inatarajia kuanza kuendesha mikutano ya baraza la madiwani katika maeneo ya Kata katika Mwaka wa fedha 2017/2018.
Kuanza kuendeshwa kwa baraza la madiwani katika maeneo tofauti ya kata kutatoa fursa kwa wananchi kuweza kushiriki na kufuatilia kwa ukaribu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri ya wilaya na kuwapa nafasi ya kuweza kuuliza maswali.
Uamuzi huu umefikiwa kutokana na Kata nyingi za Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kuwa maeneo ya mbali na makao makuu hivyo kufanya baadhi ya wananchi kushindwa kuudhuria vikao vya baraza la madiwani na kufuatilia na kujifunza mambo mbalimbali.
Awali Halmashauri ilikuwa inatumia vyombo vya habari katika kuwajulisha wananchi juu ya uwepo wa mkutano wa baraza la madiwani katika Halmashauri pamoja na kualika vyombo vya habari ili kuweza kutoa taarifa kwa wananchi utaratibu ambao utaendelea wakati mabaraza yakifanyika kwenye maeneo ya kata li kuijulisha jamii masuala mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa