Kupata "Salary Slip" kwa njia ya kieletroniki
Kupata hati ya Mshahara kwa njia ya kieletroniki (Electronic Salary slip)
Unaweza kupata salary slip kwa namna mbili tofauti:
1: WATUMISHI PORTAL
Ili kupata Hati ya Mshahara kwa njia ya kieletroniki unatakiwa kujisajili kwenye Mfumo wa Watumishi Portal. Kwenye mfumo huu wa watumishi utakuwezesha kupata taarifa zako za kiutumishi.
Vitu vya kuzingatia:
Fahamu Majina yako kamili
Hakikisha una baruapepe, kama huna utalazimika kufungua
Fahamu CHECK NO. namba yako
Ili kujisajili Bofya hapa.Kujisajili kwenye mfumo
2: GOVERNMENT SALARY SLIP PORTAL
Pia unaweza kupata hati yako ya mshahara kwa kutumia mfumo mpya wa "Government Salary Slip Portal" ambapo utajisajili kwenye mfumo.
Kwenye Mfumo huu vitu vya kuzingatia ni:
Check namba ya mtumishi
Majina kamili kama yalivyo kwenye mfumo wa Rasilimali Watu yaani HCMIS maarufu kama Lawson.
Tarehe ya kuzaliwa.
Vote Code, Sub Vote Code, Namba ya Akaunti ya Benki unayopitishia mshahara.
Fahamu pia Salary Scale, Salary Grade na Salary Step.
Barua pepe (Email) inayofanya kazi.
Ili kujisajili Bofya https://salaryslip.mof.go.tz/Manage/EmployeeRegistration
au kuingia kwa waliojisajili kwenye Government Salary Slip Portal Bofya https://salaryslip.mof.go.tz/Account/Login?ReturnUrl=%2F
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mtaa wa Idundilanga,Barabara ya Songea,Karibu na NMB.
Anuani ya Posta: S.L.P 547 Njombe
Namba ya Simu: +255 26 2782111
Simu Kiganjani:
Barua pepe: ded@njombedc.go.tz
Haki Miliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. Haki zote zimehifadhiwa